Nchi ya Burundi imeridhia kupokea chanjo ya Covid 19 huku Serikali ikisisistiza suala la kutokuwahamasisha wananchi wake kwenda kuchanja chanjo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Afya, Dkt Thaddée Ndikumana amesema kuwa chanjo hizo zimependekezwa na Benki ya Dunia na ndipo wakachukua uamuzi wa kuziingiza nchini.

“serikali haitahamasisha watu kuchoma chanjo, bali kila atakayehitaji ataifuata chanjo hii,” Amesema Waziri Ndikumana.

Hata hivyo Mamlaka ya Burundi wamekuwa na wasiwasi kuhusu kupokea chanjo hizo, ambapo hapo awali walisema watafuatilia ufanisi wa chanjo katika maeneo mengine, kabla ya kuzikubali.

Hali kadhalika Waziri Ndikumana amethibitisha ripoti ya kuongezea kwa maambukizi ya virusi vya uviko 19 katika wilaya za kaskazini zilizo maeneo ya mpakani na Rwanda, na mji wa kibiashara wa Bujumbura.

Aidha Serikali imeadhimia kufungua vituo vya tiba katika mikoa iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo.

Wizara ya afya ya Burundi hadi sasa imeripoti maambulizi karibu 6,000 vya Covid tangu janga hilo lilipoingia nchini humo mwezi Machi 2020.

Serikali kutumia Bilioni 1 na Milioni 15 kupeleka mawasilino Mbogwe
Waziri mkuu mpya wa Haiti atoa ahadi ya uchaguzi wa haraka