Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo Flava, Ruta Bushoke amefunguka kuhusiana na mipango  atakayo jishughulisha nayo katika kusongesha maisha kwa mwaka 2017.

Bushoke amesema mwaka huu amejipanga zaidi katika kazi zake za muziki na kujikita kwenye biashara ya kilimo na ufugaji kwani hiyo ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu lakini kwa mwaka huu ameamua kuchukulia hatua ndoto zake kimatendo zaidi kuhakikisha zinatimia.

“Nimepanga niwe mkulima na mfugaji ambaye mwisho wa siku naweza kujivunia pia upande mwingine wa kazi ninayofanya,” amesema. “Nataka niwe mkulima na mfugaji, 2017 nataka mwaka niwe hivyo Mungu anipe tu uzima,” ameongeza.

Kuhusu muziki, muimbaji huyo amesema, “2017 nataka niwape mashabiki wangu muziki mzuri, najua wamekumbuka  sana kusikia kazi zangu kama sasa hivi nina kazi ambayo inafanya vizuri ambayo nimemshirikisha Maua Sama inaitwa ‘Tupendane Sasa’ na bado kuna kazi nzuri nimeshafanya watazisikia.” alisema Bushoke.

Video: Mtatiro aibua madai ya wizi wa fedha CUF, ataja waliohusika
Je, ni sawa kwa wanandoa kupokea simu ya mume/mke

Comments

comments