Sherehe moja ya harusi imegeuka ajali baada ya bwana harusi mwenye umri wa miaka 31 kukimbizwa hospitalini kwa kuvunjika uti wa mgongo wake baada ya marafiki zake bwana harusi huyo kumrusha hewani na kuacha kumdaka wakimuacha akiangukia kichwa chake.

Kisa hicho kilitokea katika harusi moja kaunti ya Bihor, Kaskazini Magharibi mwa Romania wiki moja iliyopita ambapo Bwana harusi aligeuka kuwa mgonjwa katika hafla yake ya harusi baada ya kuangukia kichwa chake.

Kwa mujibu wa The Sun, bwana harusi huyo aliporushwa hewani mara ya kwanza, alidakwa lakini katika jaribio la pili aliangukia kichwa na kumsababishia jeraha baya.

Inaelezwa kuwa marafiki hao walimubeba haraka na kumuweka kwenye gari, hatua ambayo madaktari walisema ilifanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Video fupi iliyokuwa inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha bwana harusi huyo akiangukia kichwa chake katika hali ya kushangaza.

Kwa mujibu wa Daktari wa hospitali ambayo bwana harusi huyo amepelekwa kwa ajili ya matibabu amezungumzia hali yake ambapo amesema kuwa, “Mgonjwa aliumia uti wake wa mgongo. Anaendelea vizuri japo pole pole. Amelazwa katika chumba cha kufanya upasuaji wa kichwa na wiki ijayo atafanyiwa uchunguzi zaidi.”

Baraza aitangazia vita Young Africans
Matola awatuliza mashabiki Simba SC