Wananchi wanaoishi jirani na bwawa la nyumba ya Mungu lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuondoka haraka kutokana na kujaa maji na kufikia mita 688,91 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa bonde la maji la mto Pangani, Segule Segule amesema kuwa bwawa hilo kwa sasa tayari limeshafikia kiwango cha ujazo unaotakiwa ambapo kwa kawaida ukifikia lazima litoroshe maji.

Amesema kuwa maji hayo yasipotoroshwa mapema athari zake ni kubwa kuliko kwani yanaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye makazi ya watu.

“Tunaruhusu maji yatoroke kwani tusipo yaruhusu yanaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye vijiji vinavyolizunguka na kuleta maafa kwani maji hayazuiliki” amesema Segule.

Ameeleza mvua zilizoanza kunyesha mwishoni mwa mwaka jana na kuunganisha hadi mwaka huu zilijaza bwawa na kuna dalili ya kunyesha mvua nyingi Zaidi hivyo wametoa taarifa kwa wenzao wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco), kuongeza uzalishaji wa umeme ili maji yaendelee kupungua katika bwawa hilo.

Hata hivyo amebainisha kuwa timu ya wataalamu wa bonde hilo wapo katika maeneo ya bwawa kufanya utafiti kama mvua zitaendelea wanaweza kudhibiti vipi bwawa hilo lisiathiriwe.

Kaya masikini zaidi ya milioni moja kusaidiwa na Tasaf
Mwanamke aliyejaribu kufungua mlango wa ndege ikiwa angani atupwa jela