Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, kwa tiketi ya ACT- Wazalendo, Suleiman Bungara maarufu ‘Bwege’, anatarajiwa kumnadi mgombea urais wa Kenya kupitia muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga.

Bungara ‘Bwege’ amekuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka Tanzania kupewa heshima hiyo na Timu ya Kampeni ya Azimio la Umoja.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi, Janeth Rithe, imeeleza kuwa ‘Bwege’ ameshaondoka kuelekea nchini Kenya.

Uchaguzi wa Kenya unatarajiwa kufanyia Agosti 9 Mwaka huu, ambapo mpinzani mkubwa wa Raila Odinga katika Uchaguzi huo ni Naibu Rais William Ruto.

Kura mbali mbali za maoni zilizofanyika nchini Kenya, zinaonyesha Raila Odinga, anayeungwa mkono na Rais Uhuru Kenyata, amemuacha mbali Ruto.

Hotuba za mbuge ‘Bwege’ ndani na nje ya Bunge la Tanzania zinafuatiliwa na kupendwa Nchini Kenya, hali iliyomfanya apate mialiko kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini humo, Kati ya mwaka 2020-2022.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo August 5, 2022    
Kigogo afungwa karne moja jela kwa unajisi