Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu kama Bwege amesema kuwa Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe hajafanya kosa lolote na kusema kuwa kama makosa ameyafanya yeye.

Bwege amesema Zitto hana makosa kwa kuwa alimualika jimboni  kwake kuzungumza na wananchi na si kuandaa mkutano

“Kama makosa ninayo mimi niliyemualika Zitto, Pale hakuna kesi yoyote ngoja tuone huo uchunguzi wao utasema nini,” amesema Bwege

Hivyo amemtaka Zitto kutokuwa na wasiwasi wakati wakisubiria uchunguzi wa Polisi ukamilike.

Ambapo tayari Jeshi la Polisi limemfungulia jalada Zitto na kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizoripotiwa na Waziri Kangi Lugola ambaye alimtaka ajisalimishe jeshi la pilisi kwa kutoa lugha za uchochezi wakati akihutubia hadhara mkoani Lindi jimbo la Kilwa Kusini la mbunge Bwenge pindi alipoalikwa kama.

Aidha tayari Bungara amefanyiwa mahojiano na polisi na kueleza namna alivyohojiwa Julai 30, 2018  siku moja baada ya kufanyika kwa mkutano huo katika viwanja vya Garden ya Mkapa Kilwa Masoko.

Amesema polisi walimhoji mambo mawili, “kwanza ni kwanini alimualika  Zitto kuhutubia mkutano wangu wakati si mbunge wa eneo hilo. Waliniuliza njia niliyotumia kumualika, nikawajibu nilimuandikia  barua.”

“Niliwaeleza kuwa Zitto alikuja kama mbunge mwenzangu na sio kiongozi wa chama. Walinieleza kuwa sikufuata utaratibu kwa sababu kibali changu cha mkutano sikueleza ujio wa Zitto.”

Hata hivyo jana Agosti 1, ACT ilitoa tamko lake la kupinga wito wa Waziri Lugola na kusubiria wito wa Jeshi la Polisi ambao tayari wamefungua jalafa kuchunguza kesi ya uchochezi inayomkabili na endapo atakutwa na hatia, limesema Zitto atatakiwa kuripoti kituo cha polisi Kilwa mara moja.

Kesi ya viongozi wa Chadema yapigwa kalenda
Jamie Vardy, Harry Maguire kuikosa Man Utd Agosti 10