Klabu ya AS Vita kupitia kwa Rais wake, mwanamama Bestine Kazadi amethibitisha kuwa mashabiki 3000 wataruhusiwa kuhudhuria mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ‘CAF’ dhidi ya Al Ahly utakaochezwa kesho Jumanne (Machi 16).

AS Vita Club watakua wenyeji wa mchezo huo wa mzunguuko wanne wa ‘KUNDI A’ katika uwanja wa Stade des Martyrs, mjini Kinshasa, DR Congozo.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 57, amethibitisha taarifa za kuruhusiwa kwa mashabiki 3000 wa AS Vita Club kwenye mchezo dhidi ya Al Ahlky kupitia RTNC ya DR Congo.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakua wa kwanza msimu huu kwa AS Vita Club kucheza nyumbani na mashabiki, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuifunga Al Ahly.

‘CAF’ wameruhusu mashabiki 3000 kushuhudia mchezo huo, huku wakiizuia Simba SC ya Tanzania kucheza bila mashabiki kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo kwa msimu huu 2020/21.

Klabu nyingine iliyopewa ruhusa ya kuingia mashabiki uwanjani ni Al Hilal ya Sudan, ambapo CAF imeruhusu mshabiki 1000 kushuhudia mchezo wa timu yao dhidi ya CR Belouizdad utakaochezwa kesho Jumanne (Machi 16).

Wachezaji AS Vita watangaziwa ahadi nzito
CAF: Agab, Bakhit ruhsa kucheza Al Merrikh