Shirikisho la Soka Afrika CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania katika Uwanja wa Taifa wa nchi hiyo jijini Praia, Oktoba 12,2018.

Taarifa iliyotumwa na afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF, Cliford Mario Ndimbo imeeleza kuwa kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Drissa Kamory Niabe.

Ndimbo amemtaja mwamuzi msaidizi namba 2 Baba kuwa ni Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.

Aidha, mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti.

Mwamuzi wa katikati atakuwa Souleiman Ahmed Djama na Mwamuzi msaidizi namba moja Farhan Bogoreh Salime, Mwamuzi msaidizi namba 2 Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.

Kamishna wa mchezo anatokea Malawi Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda Michael Gasingwa.

Chadema kula sahani moja na mawaziri walioshiriki kupiga kampeni
Mwamuzi Ali Nassoro kuamua Shelisheli Vs Afrika Kusini

Comments

comments