Shirikisho la soka barani Afrika CAF limewafungia kwa miezi mitatu waamuzi wawili pamoja na msaidizi mmoja, kufuatia viwango duni walivyovionyesha wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 iliyochezwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Waliofungiwa ni mwamuzi kutoka nchini Ghana Joseph Lamptey aliyechezesha mchezo kati ya Afrika Kusini dhidi ya Senegal ambao walikubali kufungwa mabao mawili kwa moja.

Kosa lililomtia hatiani mwamuzi huyo, ni kutoa adhabu ya penati kwa Afrika kusini ambayo iliwapa bao la pili na la ushindi.

Mwamuzi kutoka nchini Kenya Davies Omweno ambaye alikataa bao la Libya, ambao walikubalia kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Tunisia.

Mwamuziu msaidizi katika mchezo huo Berhe O’Michael kutoka nchini Eritrea, amehukumiwa baada ya kunyanyua kibendera kuashiria offside ambayo haikuwa sahihi katika mchezo huo.

Pia shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetoa onyo kwa mwamuzi msaidizi kutoka nchini Rwanda Theogene Ndagijimana.

Bruce Arena Abebeshwa Mzigo Marekani
Lema agonga mwamba tena mahakamani