Klabu ya Bournemouth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, imekataa kufanya biashara na wagonga nyundo wa jijini London (West Ham Utd) waliowasilisha ofa ya Pauni milioni 25, kwa lengo la kuwasajili Callum Wilson pamoja na Matt Ritchie.

The Hammers, wameonyesha lengo la kutaka kuwasajili wawili hao, baada ya kukunwa na uwezo wao mkubwa waliouonyesha katika kipindi chote cha msimu wa 2015-16, uliofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita.

Uongozi wa klabu ya Bournemouth, iliyopanda daraja msimu uliopita, umeona kuna haja kwa West Ham Utd kuonyesha umakini katika ofa yao kwa kuongeza kiasi cha pesa ambacho kitaendana na thamani ya wachezaji hao wawili.

Wilson, alikua chachu ya kuisaidia Bournemouth kupanda daraja msimu wa 2014-15, kufuatia mabao yake muhimu aliyoyafunga.

Callum Wilson scored a hat-trick as Bournemouth won 4-3 at West Ham earlier in the seasonCallum Wilson pamoja na Matt Ritchie wakiwa katika mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya West Ham Utd.

Pia Wilson, alifanikiwa kufunga mabao matatu pekee yake (hat-trick) katika mchezo wa ligi kuu uliowakutanisha na West Ham Utd kwenye uwanja wa Upton Park mwezi August mwaka 2015 ambapo The Poppies walishinda mabao 4-3 huku bao lingine katika mpambano huo likipachikwa wavuni na Matt Ritchie.

Paris Saint-Germain Kumrejesha Nyumbani Anthony Martial
Borussia Monchengladbach Waisubiri Ofa Ya Arsenal

Comments

comments