Kamati ya chama cha soka nchini Cameroon, imetangaza nafasi ya kazi kwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchini hiyo.

Nafasi hiyo imetangazwa baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Hugo Broos,kumaliza mkataba wake mwezi uliopita .

Hugo Broos, ambaye alifanikisha Cameroon,kuchukua ubingwa wa mataifa ya Afrika mwaka 2017, ameondoka baada ya kushindwa kuingoza timu hiyo kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazo fanyika Urusi, 2018.

Aidha, kocha huyo alishutumiwa kuwaacha baadhi ya wachezaji muhimu sambamba na kukataa kuweka makazi yake nchini humo.

Chama cha soka nchini humo Fecafoot, kimeamua kutafuta kocha kutoka Afrika au nje ya Afrika ambaye ana rekodi ya kushinda vikombe kwenye timu yake ya taaifa na klabu enzi akiwa mchezaji na awe tayari kuishi nchini Cameroon.

Hata hivyo, Mabingwa hao walio shinda mara tano mataifa ya Afrika, wametangaza kuwa timu hiyo itasimamiwa na Alexandre Belinga kwa muda mpaka pale atakapo patikana kocha wa kudumu.

Moise Katumbi atangaza kugombea Urais
Orodha ya wenyekiti na makamu wenyekiti kamati ya kudumu ya bunge 2018-2020

Comments

comments