Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi hadharani tofauti na hapo awali ambapo iliwabidi wananchi kutumia kwa kujificha.

Sheria hiyo hatimaye ilishinda kwa kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani, huku kura 29 za maseneta zikisema hapana Sheria hiyo inasimamia udhibiti, usambazaji na uuzaji wake.

Aidha, kwasasa raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001.

Vile vile kutokana na kupitishwa kwa sheria hiyo sasa itayalazimu Majimbo, Manispaa na Mamlaka kutengeneza masoko mapya ya kuuza bangi.

Hata hivyo, Umri unaoruhusiwa kununua na kutumia bangi umepitishwa kwa mjibu wa sheria hiyo kwamba ni kuanzia miaka 18, lakini baadhi ya majimbo yamependekeza umri wa kuanzia miaka 19.

Wanaopenda michezo ya 'Kompyuta' hatarini kuugua ugonjwa wa akili
Merkel, Macron wateta kuhusu mzozo wa Umoja wa Ulaya