Canada imekuwa nchi ya pili baada ya Uruguay kuruhusu kisheria matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi kwa ajili ya tiba (recreational marijuana).

Soko la nchi hiyo linalouza bangi linafunguliwa rasmi Jumatano usiku wa ‘manani’, hali inayozua wasiwasi kuhusu madhara ya matumizi hayo kiafya na kiusalama wa umma kwa ujumla. Tayari watu wameanza kununua kwenye maduka ya rejareja wakipewa risiti zilizokatwa kodi.

Picha ya wanaodaiwa kuwa wa kwanza kununua marijuana katika eneo la St. John’s Newfoundland

Taarifa za sheria hiyo mpya imetumwa kwa wakaazi zaidi ya milioni 15 kwa ajili ya kuwajulisha wananchi pamoja na kufanya kampeni ya udhibiti wa matumizi yake kwa tiba.

Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kupitisha sheria ya kuruhusu matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa ajili ya tiba, ingawa Ureno na Netherland walikuwa wametangaza kuwa matumizi ya bangi sio kosa la jinai.

Majimbo ya Canada yalikuwa kwenye vuguvugu la kujiandaa kuondoa katazo la matumizi ya mmea huo.

Majimbo hayo kupitia sheria hii mpya yamepewa jukumu la kuandaa taarifa ya kina ya namna bangi itakavyokuwa inanunuliwa au kuuzwa pamoja na kanuni za udhibiti wake kwa ajili ya matibabu.

Serikali yasimamisha huduma hospitali za Marie Stopes
Ni kweli Chadema tunachangishwa, lakini sio sababu ya kuhama- Mbunge Meiseyeki