Bingwa wa dunia wa masumbwi ya uzito wa kati, Canelo Alvarez ametangaza kutoshiriki pambano la marudiano kati yake na bingwa mwenzake, Gennady Golovkin maarufu kama ‘Triple G’.

Pambano la marudiano kati ya wababe hao lilipangwa kufanyika Mei 5 mwaka huu, kufuatia pambano la awali ambalo walitoka sare huku wengi wakiamini Triple G alistahili kuwa mshindi.

Canelo amechukua uamuzi huo baada ya vipimo alivyofanya mara mbili kuonesha kuwa alitumia dawa zisizoruhusiwa kwenye michezo.

Hata hivyo, promota wa pambano hilo amesema kuwa ingawa Canelo amejiondoa kwenye pambano hilo, Tripple G atapambana siku hiyohiyo na bondia mwingine ambaye watamtaja hivi karibuni.

Kuahirishwa kwa pambano kati ya wawili hao kunamfanya Triple G kuwa katika wakati mgumu wa kumpata mpinzani ambaye atakuwa na uwezo wa kuvuta dili la $27.06 milioni ambazo alikuwa anapata kupitia pambano lake na Canelo.

Triple G hajawahi kushindwa pambano huku akitoa sare na Canelo, lakini Canelo amewahi kupoteza pambano moja tu dhidi ya Floyd Mayweather na kutoa sare mbili.

Museveni azungumza na Askofu Mkuu kuhusu tuhuma za 'kumpindua'
Video: Wabunge upinzani watofautiana bungeni, Mbowe atoka na msimamo mkali Segerea