Mlinzi wa Tanzania, Nadir Haroub ‘ Cannavaro ‘ amesafiri na kikosi cha Taifa Stars kwenda Nairobi, Kenya kucheza na wenyeji Harambee Stars mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Cannavaro ni mmoja wa wachezaji 25 wa Taifa Stars waliondoka saa 12.00 Alfajiri kwa ndege ya FastJet.

Awali iliripotiwa kuwa Cannavaro amegoma kuitikia wito wa kujiunga na Kikosi cha Taifa Stars kutokana na kutofurahishwa na kitendo cha kuvuliwa unahodha wakati akiwa majeruhi.

Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu hawamo kwenye msafara huo kutokana na kukabiliwa na majukumu ya vilabu vyao nchini Ubelgiji na JK Kongo.

Pambano dhidi ya Kenya litakalochezwa Jumapili ni maandalizi ya kujiandaa kucheza dhidi ya Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Msafara wa Taifa Stars unajumuisha kikosi cha wachezaji 25, watu nane wa benchi la ufundi wakiongozwa na makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco na mkuu wa msafara.

Kikosi kilichoondoka:

Walinda Milango: Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam) na Benny Kakolanya (Prisons).

Walinzi: Mwinyi Haji, Nadir Haroub na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam) Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).

Viungo: Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui).

Washambuliaji: Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Prisons).

Mourinho Adhamiria Kuwafundisha Adabu Chelsea
Mrema: Maalim Seif akamatwe