Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itacheza mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Cape Verde Oktoba 12, 2018 na mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Taifa Oktoba 16, 2018.

Afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kwa kushirikiana na Wadhamini wa Taifa Stars Bia ya Serengeti Premium Lager inafanya utaratibu wa usafiri utakaoipeleka na kuirudisha timu ya Taifa kulingana na ratiba ya michezo hiyo ilivyokaa.

Ndimbo amesema utaratibu wa Kambi/Kikosi Walimu watauzungumza ambao utazingatia umuhimu wa mchezo,tarehe za kuondoka na tarehe za michezo yote miwili.

“Unafanyika utaratibu wa kusafiri na mashabiki wa timu ya Taifa ambao watachangia gharama kidogo.”

“Tumekuja na Hashtag itakayotumika katika safari yetu ya kutupeleka Cameroon kwenye fainali hizo za mwakani, #AfconCameroon2019ZamuYetu.” Amesema Ndimbo katika mkutano na waandishi wa habari.

“Rai yetu kwa Vyombo vya Habari tuungane pamoja kwakuwa ni sehemu muhimu katika safari hiyo ya kwenda Cameroon,Wadau mbalimbali tuungane pamoja Tanzania ni yetu,Taifa Stars ni timu yetu.”

Msimamo ulivyo mpaka sasa Taifa Stars ina nafasi ya kwenda Cameroon kwenye Fainali za Afcon.

Uganda wanaongoza wakiwa na alama 4 ,Lesotho na Tanzania wana alama 2 na Cape Verde wakiwa na alama 1.

#AfconCameroon2019ZamuYetu

Nandy afunguka kuhusu kuacha muziki
Bodi ya ligi kufanya uchaguzi