Cardi B ameamua kumburuza mahakamani mwandishi maarufu wa habari za udaku, Latasha K akimtuhumu kumchafua kwa habari za uongo.

Kwa mujibu wa TMZ ambao wamesema wameona nyaraka za maelezo ya rapa huyo wa kike, malalamiko yake yanatokana na video 23 za mwandishi huyo zinazomuonesha akimshambulia vikali ndani ya kipindi cha miezi 14 iliyopita.

Latasha alidai kuwa Cardi B alimharibu mwanaye akili kwani alikuwa akitumia madawa ya kulevya wakati wa ujauzito wake.

Kadhalika, Cardi B anamshtaki pia mwandishi Ebony Jones ambaye aliweka mtandaoni video ambazo zinamshambulia akitaja majina ya dawa za kulevya amnbazo alikuwa akitumia ikiwa ni pamoja na cocaine. Zaidi, Jones alidai kuwa rapa huyo ana magonjwa ya zinaa anayoyasambaza makusudi.

“Yaani kahaba aliyetajwa kuwania tuzo za Grammy anazunguka kila mahali akisambaza magonjwa yake ya zinaa (herpes),” alisema Jones.

Katika maelezo yake, Cardi B ameeleza kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya zilizotajwa na Latasha na Jones, na kwamba hana ugonjwa wowote wa zinaa.

Alisema kuwa ameshawapa wawili hao nafasi ya kumuomba radhi lakini hawakutekeleza. Hivyo, ameamua kuwachukulia hatua za kisheria.

Cardi alipata mtoto wake wa kike aliyemuita Kulture, aliyempata na Offset.

Video: Jibu la Rais Magufuli kuhusu kuifanya leo kuwa siku ya mapumziko
JPM atoa zawadi ya viwanja kwa wachezaji wa Taifa Stars

Comments

comments