Msanii wa Marekani rappa Cardi B amepagawa na muziki wa Afrika baada ya Somadjozi kushinda tuzo ya Best New Art, International Act, amesema kuwa ameshangazwa na jinsi Afrobeats inavyoteka Marekani.

Kupitia Insta story yake rapa huyo amefunguka namna anavyofurahi kuona muziki wa Afrobeats ukikua kila kukicha, ametolea mfano furaha alikuwnayo Somadjozi kutoka Afrika Kusini hadi akaanza kulia baada ya kushinda tuzo ya Best New Art, International Act katika usiku wa tuzo za BET Awrads jana.

Tuzo hizo ambazo zilifanyika katika ukumbi a Mcrosoft Thearter jijini Los Angeles  Marekani, Cardi B ameibuka na tuzo ya Best female HipHop  Artist mwaka 2019 huku akiongoza kwa kutajwa katika vipengele saba.

Hata hivyo rapa huyo ambae ameteka soko la HipHop tayari ameshilikishwa kwenye baadhi ya nyimbo na wasanii wa kubwa nchini humo akiwemo Dj Khalid, Bruno Mars na wengine wengi.

Aidha mtoto wa rapa Cardi B aliyezaa pamoja na rapa offeset kutoka katika kundi la Migoes anaejulikana kwa jina la Kulture anatarajia kutimiza mwaka mmoja Julai 10 mwaka huu na amesha ahidiwa zawadi za gharama na wazazi wake hao.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ  umeripoti kuwa Cardi B na Offset wamepanga kumpendezesha mtoto wao kwa vito tha thamani mwilini, Sonara aliyepatiwa kazi hiyo Elliante amesema kuwa Cardi B amelipa kiasi cha Tsh millioni 220 ambapo hafla hiyo itagharimu  kiasi cha $400k sawa na Tsh millioni 900.

 

Msanii maarufu aliyedai kuwa na dawa ya Ukimwi akamatwa
Apatwa na ndoto za kutisha baada ya kujikuta pekeyake kwenye Ndege