Rapa maarufu nchini Marekani Cardi B ambaye ni mama wa mtoto mmoja amekiri kuwahi kutumia madawa ya kulevya kulewesha wanaume na kuwaibia kipindi anafanya kazi ya stripper katika maeneo tofauti ya starehe.

Cardi B ametoa kauli hiyo kupitia kipande cha video alichowahi kujirekodi katika Mtandao wa instagram na kinaripotiwa kuwa ni cha zamani kidogo, na kueleza kuwa malalamiko hayo yamewafikia wanaume ambao wamedai kuwa Cardi B anafaa kuchukulia hatua  kali kwa alichokuwa anakifanya na anapaswa kwenda jela.

Aidha video hiyo ambayo imeamsha hasira za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii huku wakimtuhumu rapa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokuwa anakifanyana na kuomba serikali kumchukulia hatua za kisheria.

Survingi Cardi B ndio kipande cha video iliyosambaa kwenye mitanado ya kijamii kwa baadhi ya mashabiki huku wengi wakiunga mkono rapa huyo kuchukuliwa hatua.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Tweeter amesema kuwa “Inakupasa kufanya kazi nzuri ili ulete mkate juu ya meza, watu wanasahau kuwa nilifanya hivyo kwaajili ya maisha yangu na ili kuwa hai iliniladhimu kuwa stripper, ndio niliwalewesha na kuwaibia hicho ndicho nilichokuwa nikifanya ”.amesema Cardi B.

 

 

Safu ya uongozi wa klabu ya Yanga yaachia ngazi
Spika za masikioni chanzo cha Saratani

Comments

comments