Rapa wa kike Cardi B jana alifanikiwa kujifungua mtoto wake wa kwanza wa kike aliyempata na rapa Offset.

Cardi ameweka  hadharani habari hiyo njema leo kupitia Instagram, akiambatisha jina halisi la mwanae huyo pamoja na picha aliyopiga mtupu wakati wa ujauzito.

“Kulture Kiari Cephus 7/10/2018 @offsetyrn,” aliandika Cardi B.

Hii ina maana kuwa mtoto wake anaitwa Kulture. Jina halisi la baba yake (Offset) ni Kiari Cephus.

Offset ambaye ni mwanafamilia wa kundi la Migos, alifunga ndoa kwa siri na Cardi, Oktoba mwaka 2017. Cardi aliweka wazi kuwa ana ujauzito alipokuwa anafanya mahojiano na ‘Saturday Night Live’.

Baadaye alipiga show kwenye tamasha la Coachella lakini alilazimika kusitisha ziara yake kutokana na hali ya ujauzito.

Kulture anakuwa mtoto wa nne wa Offset. Hongera kwa familia hii ya wana hip hop/rap.

Mbunge aongoza maandamano ya kupinga kodi ya mtandaoni Uganda
Steve Nyerere: Msiba wa Patrick ni wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi

Comments

comments