Meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, Carlo Ancelotti ameendelea kusisitiza suala la kuondoka kwa kiungo Mario Gotze.

Ancelotti alisisitiza uhakika wa kuondoka kwa kiungo huyo wakati huu wa majira ya kiangazi, alipozungumza na vyombo vya habari katika hafla ya kutambulishwa kwake, iliyofanyika jana mjini Munich.

Meneja huyo kutoka nchini Italia, alisema pamoja na kiungo huyo kuendelea kuwepo klabuni hapo, bado kuna uwezekano wa kuondoka na kwenda mahala pengine kucheza soka lake.

Alisema siku chache baada ya kuwasili mjini Munich, alizungumza na Gotze na kumueleza baadhi ya mambo ambayo hakuwa tayari kuyaweka wazi, na ana uhakika mchezaji huyo atayafanyika kazi.

“Pamoja na kuendelea kuwepo hapa, bado nitamtumia kama mchezaji wa hapa katika kipindi cha maandalizi ya msimu ujao, na ikitokea anaondoka nitamruhusu kufanya hivyo.”

“Nimefanya mazungumzi na Gotze, lakini sitokua tayari kusema ni nini tulichokubaliana kutokana na jambo hilo kuwa siri baina yetu.” Alisema Ancelotti ambaye anachukua nafasi ya Pep Guardiola aliyetimkia Man city.

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani na Tottenham Hotspurs ya England zinachuana kuiwania saini ya Mario Gotze.

Hata hivyo Acelotti, alizungumzia mazingira ya klabu hiyo kwa kusema amependezwa nayo, na ana uhakika wa kutimiza malengo yanayokusudiwa na viongozi wa FC Bayern Munich.

“Naamini kikosi kipo vizuri. Ila sitazungumzia suala la usajili kwa sababu bado dirisha lipo wazi hadi Ogasti 31, Kwa sasa naomba nizungumzie wachezaji waliopo kikosini tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.” Aliongeza Ancelotti.

Mwenyekiti wa FC Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, jana alichukua jukumu la kumtambulisha Ancelotti mbele ya waandishi wa habari pamoja na kumtembeza sehemu za uwanja wa Allianz Arena.

Aldo Agroppi: Nashangaa Kuona Klabu Inajipangia Ada Ya usajili
Gwajima anasa mikononi mwa polisi, simu zake zapekuliwa