Wakati Argentina wanapewa uenyeji wa Kombe la dunia 1978 walihitaji utulivu mkubwa kwenye Jiji la Buenos Aires,  ndipo Dikteta Juan Carlos Ongania aliagiza maskini wore watolewe katikati ya jiji na kupelekwa Barrio Ejercito do Los Andes ‘Fuerte Apache’ mnamo 1966.

Miaka 18 baadae anazaliwa Carlos Alberto Martinez baadae anabadili jina na kuitwa Carlos Tevez kuepusha ugomvi kati ya klabu, Old Boys na Boca Juniors, alizaliwa kwenye mitaa ya Ciudadela ila alienda kulelewa na Mama yake mkubwa, Adriena Naoemi Martinez.

Ndipo hapo Fuerte Apache Tevez alijifunza uhuni, udokozi na ukorofi, kila aina ya matukio mabaya yalipatikana Fuerte Apache, ilipelekea Tevez kuvunja meno yake ya mbele na kumwagiwa maji kupelekea kovu analodumu nalo maishani.

Kovu lake linaakisi maisha halisi ya watu wa Apache, Watabibu watatusaidia ila ile ni 3rd degree burn, lakini Tevez aligoma kufanyiwa upasuaji wakutoa kovu, aliamini ni alama yake kutokea mitaa iliyomlea.

Tevez aliliteka soka la Amerika Kusini, Boca Juniors, Corinthians na baadae barani Ulaya pale West Ham, United na City kisha Juventus, ni Tevez huyu aliweka kambani pale Etihad kisha akavua jezi kuonesha jina FUERTE APACHE, ni Tevez huyu aliyesepa Ulaya kurejea Boca Juniors ili awe karibu na Fuerte Apache.

Wahuni mtaani wakampachika jina El Apache ,yani yeye ndio alama ya mtaa wao ni Tevez mtu muhimu kwao na nembo yao licha ya dharau za Dikteta Ongania na taswira ya Apache.

Ufikapo usimtaje Lionel Messi wa Rosario, wao Mfalme wao ni Tevez aliyekuwa kwa moshi wa sigara, ufikapo Apache hisi upo Bogotá Columbia, Santiago Chile na Montevideo pale Uruguay, wana style zao na utamaduni wao.

Unaweza ukatutoa nje ya mtaa, ila abadani huwezi ukaitoa mitaa mioyoni mwetu!  TEVEZ REMEMBER THE NAME.

Ubalozi wa China umetoa misaada ya vifaa kinga ili kukabiliana na mlipuko wa Corona Tanzania
Ummy: Viongozi wa dini epukeni misongamano wakati wa Pasaka