Shirikisho la soka nchini Brazil (CBF) limemfukuza kazi kocha Carlos Dunga baada ya matokeo mabaya kwenye michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani.

Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil (The Selecao) kilitolewa kwenye hatua ya makundi  ya mashindano hayo baada ya kutoa sare na Ecuador na kufungwa na Peru, licha ya kushinda 7-1 dhidi ya Haiti.

Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa Corinthians, Tite, ambaye ataiongoza timu hiyo katika michuano ijayo ya Olimpiki nchini Brazil.

Dunga aliingia kwenye mashindano hayo akiwa katika wakati mgumu baada ya timu kucheza vibaya kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 na pamoja na matokeo mabaya ya Marekani, imesababisha kufukuzwa kwake.

Picha: Poulsen Na Shime Waanza Program Ya Kuwavaa Shelisheli
Wapinzani Wa Young Africans Wafikiria Kujitoa Kombe La CAF