Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini, kimesema kuwa Mbunge wa jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa ajiandae kisaikolojia kuachia jimbo hilo.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Joseph Mgongolwa ambapo amesema kuwa ushindi walioupata ni salamu tosha kwa mchungaji Msigwa, hivyo anatakiwa ajitathmini na kuangalia kazi nyingine ya kufanya.

Chama hicho kimesema kuwa hali hiyo inatokana na wimbi là madiwani wa Chadema waliohamia CCM na baada ya uchaguzi mdogo wamepoteza kata zote za Chadema.

Aidha, Katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanikiwa kushinda Kata tano bila kupingwa.

“Ule muda wa kupiga kelele umekwisha, sasa ni vitendo, Watanzania wamechoka kudanganywa, wana Iringa wamechoka ahadi hewa, wanataka mabadiliko,”amesema Mgongolwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa ushindi walioupata ni salamu tosha kwa Mchungaji Msigwa kujitafakari na kuangalia kazi nyingine ya kufanya kwa sababu hatarudi tena mwaka  2020.

 

Rais Trump: Mkiniondoa madarakani Marekani itafilisika
Kaka kufuata nyayo za Leonardo, Paolo Maldini AC Milan