Mwenyekiti wa Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Kagera, Nazir Karamagi aimeigiza SUMA JKT kuhakikisha wanamaliza mradi wa jengo la halmashauri kwa muda unaotakiwa.

Akiongea wakati wa ziara ya kamati ya siasa kwenye ujenzi wa jengo hilo la Halmashauri ya Wilayani Bukoba, Karamagi amesema ameridhishwa na hali ya ujenzi wa jengo hilo kutokana na ubora unaoonekana na kumtaka mjenzi kuongeza kasi na nguvu kazi, ili kuweza kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Aidha, kamati hiyo pia imemuomba mkurugenzi kuwapa kipaumbele vijana wanaopatikana kwenye maeneo ambayo serikali itakuwa inatekeleza miradi ili kuendelea kuwa na imaani na serikali yao

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Mhandisi Hamza Kambuga amesema kuwa ujenzi umefikia asilimia 80% na umetumia kiasi cha Zaidi ya bilioni 1.8 ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha zaidi shilingi bilioni 2.7.

Kamati hiyo pia imetembelea mradi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu milioni 150, jengo la halmashauri, vyumba vya madarasa shule ya sekondari Karamagi sambamba na kuhamasisha upandaji miti ya matunda na kufanya mikutano ya hadhara.

Katika kuikaribisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kagera inaadhimisha sherehe hizo kwa kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo kwenye wilaya zote za mkoa wa Kagera.

Azam FC yaifuata Dodoma Jiji FC
Sheikh Mkuu DSM atenguliwa