Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kagera kupitia mkutano wake wa halmashauri kuu ya mkoa kimeonyesha kuridhika na shughuli zinazofanywa na serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Katika mkutano huo uliofanyika julai 26 mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Bukoba, serikali kupitia ofisi ya mkuu wa Mkoa iliwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa ilani iliyokuwa imesheheni mambo mengi ambayo imeyatekeleza kuanzia January hadi mwezi juni mwaka huu.

Akiwasilisha taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa kwa upande wa uchumi pato la mkazi wa Kagera limeongezeka kutoka milioni 1.3 kwa mwaka 2016-2017 hadi 1.367 kwa 2017-2018 kwa mwaka sawa na ongezeko la 1% huku mchango wa mkoa katika pato la Taifa ni Trilioni 1.7 mwaka 2016-2017 hadi Trilioni 4.9 kufikia 2017-2018 sawa na ongezeko la 9%

Kuhusu makusanyo ya mapato kwa upande wa TRA mkuu wa mkoa amesema kuwa 2017-2018 mkoa umefikia makusanyo ya shilingi billioni 48.7 sawa na ongezeko la 10% kutoka bilioni 44 kwa mwaka 2018-2019 kufikia juni 30 huku upande wa halmashauri pia makusanyo yakiongezeka hadi asilimia 86 ambapo halmashauri ya wilaya Biharamulo ikionyesha kufanya vizuri zaidi .

Aidha, kuhusu zao la chakula, Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kwa msimu wa 2019- 2020, Mkoa umejiwekea lengo la kukusanya tani milioni 52 ambapo mpaka sasa wameshakusanya kiasi cha tani milioni 9.7 sawa na 20% ambapo tayari wameshapokea fedha bilioni 11.4 ambazo tayari bilioni 10 zimeshalipwa kwa wakulima.

Hata hivyo, Gaguti ameongeza kuwa katika zao hilo kumekuwepo na changamoto ya magendo ya kusafirisha Kahawa kwenda nje ya nchi na kusema kuwa mkoa umejipanga kuhakikisha changamoto hiyo inafikia kikomo.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Kagera, Benardeta Mushashu amesema kuwa ipo haja ya wananchi kupewa elimu ya kutosha juu ya mfumo mpya wa malipo japo unaweza kuwa unasumbua lakini ni salama kwa kutunza fedha zao.

Kheri James aunguruma Kagera, 'Anayempinga JPM huyo ni mkimbizi'
Wafanyakazi TRA watakiwa kufanyakazi kwa weledi