Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema chama hicho kinatarajia kufanya vikao vyake vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kikao cha kamati kuu kitafanyika Juni 26, 2019 huku kikao cha NEC kikitarajiwa kutafanyika Juni 27, 2019 na kitakuwa cha kawaida kwa mujibu wa kalenda ya chama na Katiba ya CCM ibara ya 101(2).

Polepole amesema kikao cha Kamati Kuu kikitanguliwa na vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Juni 24, 2019 na kufuatiwa na semina ya makatibu wa mikoa Juni 25, 2019.

Amesema semina hiyo itaendeshwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Philip Mangula pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati kuu ya Taifa.

Ameongeza kuwa wajumbe wa vikao hivyo watapata fursa ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya CCM ya awamu ya Tano iliyo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Video: Ni muhimu watumishi kushiriki michezo - Majaliwa
Shambulio la Septemba 11 lilivyovuta vita ya Marekani dhidi ya Afghanistan #HapoKale