Moja ya waliokuwa wanawania kupewa nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, Dkt. Muzamil Kalokola amedai kuwa atakuwa ni moja ya watu ambao wataonyesha nia ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama hicho mwaka 2020.

Kada huyo Mkongwe wa CCM, amedai kuwa moja ya sababu kubwa ambayo imemfanya aweke wazi hilo ni kwamba Mwenyekiti wao wa chama amekuwa akikiuka baadhi ya taratibu za chama hicho ikiwemo kuteua wapinzani katika nyadhifa mbalimbali.

“CCM tulijiwekea utaratibu wa kumuachia Rais kuwa mgombea pekee pale anapomaliza miaka mitano ili akamilishe mitano mingine ili kipindi chake cha miaka 10 kikamilike, lakini Rais Magufuli amekiuka misingi kwa hivyo hakuna sababu ya kumwachia, nitaomba ridhaa nipitishwe.” amesema Dk Kalokola.

Licha ya Kada huyo kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya Rais Magufuli, mwingine ambaye alikuwa ametajwa ni aliyekuwa Mbunge wa Mtama, Bernard Membe lakini taratibu za chama hicho zinakataza mtu kutangaza kuwania nafasi ambayo tayari inaongozwa na kiongozi wa chama hicho.

Dereva aliyembeba Mbuzi nyuma ya gari la umma achukuliwa hatua
LIVE MIKOCHENI: Waziri Mkuu Akizindua Chaneli ya Utalii, "Tanzania Safari Channel"

Comments

comments