Matokeo ya majimbo mengine ya mkoa wa Mara yametangazwa rasmi leo ambapo majimbo ya Mwibagi, Butiama, Tarime Vijiji na Rorya yamepata majibu ya sauti ya umma.

Kangi Lugola, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mwibala mwenye mbwembwe za aina yake awapo bungeni akitafuta haki ya wapiga kura wake ameweza kutetea nafasi yake baada ya kupata kura 33,845 na kumshinda mpinzani wake kwa mbali, Chiliko David wa Chadema aliyepata kura 6675.

Katika Jimbo jipya la Butiama, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo amemtangaza Nimrod Mkono wa CCM kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 4,7469 dhidi ya mpinzani wake mkuu, Yusuf Kazi wa Chadema aliyepata kura 14451.

Wananchi wa jimbo la Tarime Vijijini pia wamempokea John Heche wa Chadema kuwa Mbunge wao baada ya kutangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi baada ya wananchi hao kumuwezesha kupata kura 51830 dhidi ya Christopher Kangoye wa CCM aliyekuwa akimfuatia kwa kura 4591.

Wapiga kura 57914 wa jimbo la Rorya wamempa ushindi tena Lameck Airo dhidi ya Steven Juma wa Chadema aliyepa kura 42532. Lameck Airo ameweza kutetea kiti chake kwa mara nyingine na kumuwezesha kuendelea kuwawakilisha wananchi wa Rorya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mingine mitano.

Katika majimbo mengine ya yaliyotangazwa awali, Jimbo la Musoma Mjini limechukuliwa na Vedastus Mathayo (CCM), Jimbo la Tarime Mjini limechukuliwa na Ester Butiku (Chadema).

Wassira: Sikubali, Nimehujumiwa
Profesa Jay kimeeleweka Jimbo La Mikumi, Azungukwa na Madiwani wa CCM