Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewataka wanachama wake kuwa sehemu ya kutoa elimu kwa jamii pamoja na ufafanuzi juu ya uhakiki wa mali za chama uliofanyika hivi karibuni mkoani humo.

Hayo yamesemwa mkoani humo na Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho, Erasto Ngole ambapo amesema kuwa baada ya chama kufanya uhakiki wa mali zake kulitokea baadhi ya watu wenye nia ya kupotosha ukweli juu ya zoezi hilo wakisema kuwa chama kimepokea mali za Serikali.

Amesema kuwa kufuatia upotoshaji huo Wanachama wa CCM mkoani Njombe wanatakiwa kuwa sehemu ya utoaji elimu juu ya zoezi hilo kwakuwa chama kimepiga chapa Majengo, viwanja pamoja na mali nyingine ambazo ziliandaliwa na Waasisi wake enzi za chama kimoja cha TANU chini ya mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM kupitia mfumo wa Ujamaa.

‘’Vitu vyote vilivyo andaliwa wakati wa chama kimoja kupitia mfumo wa Ujamaa hivyo ni mali ya CCM, mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyekuwa Katibu mkuu wa chama chetu mwaka 1982 hadi mwaka 1990 ndiye aliyepita vijiji vyote hapa nchini na kuiwezesha TANU kuanzisha miradi mbalimbali na ndio maana leo chama kinafuatilia mali zake na kimeweka alama katika mali hizo ili baadae chama kisiingie malumbano na Taasisi nyingine,’’ Amesema Ngole

Aidha, ameongeza kuwa anaamini kuwa Kijiji cha Itulike kitaongoza kwa kishindo kikubwa katika matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu kwakuwa Kijiji hicho ni sehemu ambayo yeye anaishi hivyo nilazima ahakikishe kuwa heshima ya Chama cha mapinduzi inaanzia kijijini hapo.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi CCM mkoani humo, Juma Nambaila amewataka wanachama wa CCM mkoani humo kuendelea kujitokeza kwa wingi kufanya usajili wa kadi zao kupitia mfumo mpya wa Kielectronic ili kuachana na kadi zilizokuwa zikitumika awali zilizokuwa kwenye mfumo wa Karatasi.

Video: Janga jipya laibuka Dar, Hoja za Nassari zaibua mjadala
Dkt. Gwajima awataka Wasimamizi wa huduma za afya kuimarisha mfumo wa uwajibikaji