Siku chache baada ya kumalizika uchaguzi mkuu uliofanya mabadiliko katika jiji la Tanga baada ya Chama Cha Wanachi (CUF) chini ya mwanvuli wa Ukawa kushinda nafasi ya Ubunge na kujizolea madiwani wengi zaidi, wanachama wa CCM wamezua varangati kubwa wakiwatuhumu viongozi wao kuwa chanzo cha kushindwa kwao.

Tanga ilikuwa moja kati ya ngome kuu ya CCM tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi lakini mwaka huu hali ilikuwa tofauti na Chama Cha Wanachi CUF kiliweza kushinda Ubunge na kupata madiwani 16, idadi inayowapa nguvu ya kuwa na Meya na kuunda halmashauri.

Kufuatia hali hiyo, jana wananchi hao walikusanyika katika ofisi za chama hicho na kuwatuhumu viongozi wa ngazi za wilaya na mkoa wakidai kuwa wamekisaliti chama hicho kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Wanachama hao waliozua varangati na kutaka kuwang’oa mara moja viongozi hao wanaowatuhumu hawakuishia hapo, walidai kuwa endapo viongozi hao hawataondolewa mara moja wao watafanya maandamano makubwa kuwapinga.

“Kwa hiyo sisi tumeamua tuondoke tufuate taratibu zingine. Na hizi ni salaaam kwa Bwana Kinana (Katibu Mkuu wa CCM), sisi tuko njiani kuja, Tanga tumeanguka, tuna uchungu, tumefedheka haijawahi kutokea tokea tupate Uhuru na Chama hiki,” alisema mwanachama mmoja.

Walidai kuwa viongozi hao walifanya makosa hata katika uteuzi wa wagombea kwani waliwaweka watu ambao walikuwa na makundi katika chama hivyo baada ya kura za maoni wanachama waligawanyika na kuwapa nafasi nzuri zaidi wapinzani wao CUF, chini ya Ukawa.

Mussa Mbaruk wa CUF alitangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo huku akipata viti vya madiwani katika kata 16 kati ya kata 27 za jiji la Tanga.

Polisi Wabainisha Uhalifu Uliofanywa Na Kituo Cha Sheria, Haki Za Binadamu ‘LHRC’
Masanja Mkandamizaji Aanza Rasmi Safari ya Kuingia Bungeni