Hatimaye mchakato wa kumchagua mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM umekamilika.

Mchakato huo umewezesha Job Ndugai kuwa mgombea Uspika huku akisubiri kupigiwa kura na wabunge wa vyama vyote baada ya upande wa upinzani kutangaza mgombea wao.

Job Ndugai ameweza kuchaguliwa katika ya makada zaidi ya 21 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya kuwa kiongozi mkuu wa Bunge. Ni dhahiri kuwa Ndugai amepata uzoefu wa kutosha kutoka katika Bunge la 10 alipokuwa Naibu Spika wa Bunge hilo.

Christian Bella afanya Collabo na Koffi Olomide
Mugabe: Raila Odinga Akikanyaga Zimbabwe Nitamkamata Na ‘Kumhasi’