Chama Cha Mapinduzi Ccm kimempongeza Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika muda mfupi wa uongozi wake.
Pongezi hizo Zimetolewa kupitia Kwa Msemaji wa chama hicho Christopher Ole Sendeka Alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.                                                                                                                                           Rais Magufuli aliahidi mabadiliko. Tunampongeza kwa kusimamia vema utekelezaji wa ilani ya CCM. Katika muda mfupi wa miezi tisa tu, Rais Dk Magufuli amefanya mambo makubwa.
Sote tunafahamu kuwa Shirika letu la Ndege, ATCL, limekuwa linafanya kazi na ndege moja.lakini  Serikali ya Dk Magufuli imekwisha lipia ndege tatu za abiria toka Canada, ndege mbili zitaingiza nchini mwezi ujao alisema ”Ole Sendeka.
Aidha Ole sendeka alitaja baadhi ya maeneo ambayo raisi magufuli ni pamoja na Reli ya kati inajengwa kwa kiwango cha Standard Gauge. Meli katika ziwa viktoria inanunuliwa katika bajeti ya mwaka huu. Elimu ya msingi na sekondari inatolewa bure. Wanafunzi  sasa wanakalia madawati na kujifunza vizuri zaidi.
Ole sendeka aliongeza kuwa barabara zimeendelea kujengwa. Makusanyo ya kodi yameongezeka. Huduma za jamii zinaendelea kuimarika. Lakini pia, nidhamu katika utumishi wa umma sasa imeimarika. Wananchi wanastahili huduma nzuri na kuthaminiwa na wafanyakazi wa Umma.
Hata hivyo Mataifa mengi ya Afrika na nje ya Afrika yanaiga mbinu za Rais Magufuli katika kuleta mabadiliko nchini mwao.
                                                                                                                                          Dk. Magufuli ameazimia kujenga uchumi wa viwanda. Ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi wa kati na Maisha ya wananchi  yataboreka.
Katika hatua nyingine Ole sendeka alisema Wapo wachache wanaelekea kutafuta mbinu chafu za kuhujumu mafanikio haya, lakini hawatafanikiwa. Watanzania wamemchagua Dk. Magufuli ili awaletee maendeleo na kuwataka wananchi wawapuuze.
JWTZ kufanya usafi Mitaani Septemba 1, wasema Serikali imekataza maandamano
Ccm Wa Laani Mauaji Ya Askali Polisi Yaliyotokea Eneo la Mmbande Wilaya Ya Temeke