Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa tamko kuhusu sakata la baadhi ya wabunge wake waliokuwa katika Kamati za Bunge kufikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa taasisi za Umma.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alitoa tamko la chama hicho akidai kuwa kimepanga kuwaadhibu wabunge wote watakaokutwa na hatia katika tuhuma hizo za rushwa.

Ole Sendeka alisema chama hicho kinaunga mkono uchunguzi unaoendelea na kwamba watachukua hatua za kinidhamu kama chama dhidi yao.

Jana, wabunge watatu wa chama hicho, Kangi Lugola (Mwibara), Ahmed Saddiq (Mvomero) na Victor Mwambalaswa (Chunya) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu wakituhumiwa kupokea rushwa ya shilingi milioni 30.

Wabunge hao walifikishwa mahakamani siku chache baada ya Takukuru kuwahoji baadhi wa wabunge kuhusiana na kuwepo tuhuma za baadhi ya wabunge wa kamati za Bunge kupokea rushwa kutoka kwa taasisi mbalimbali ikipewa jina la ‘Lunch’ ili wawalinde na mkono wa Bunge.

Herve Renard Aipeleka Morocco AFCON 2017
Daraja la Juu ‘Flyover’ laporomoka na kuua makumi