Baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kumpokea rasmi waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama chake hicho cha zamani kimejipanga kurudisha mashambulizi.

CCM imepanga kufanya mkutano na waandishi wa habari leo majira ya saa 7 mchana,  Peacock Hotel, Dar es Salaam.

CCM inatarajia kutoa taarifa juu ya uamuzi wa Lowassa pamoja na mengine yanayohusu mustakabali wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu mwenzi Oktoba.

Akizungumza katika mkutato wa kujiunga na Chadema jana jijini Dar es Salaam, Edward Lowassa aliituhumu CCM kwa kumuonea na kulikata jina lake bila kuzingatia matakwa ya katiba, wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho uliokamilika kwa kumtangaza Dkt. John Magufuli.

Lowassa alisema kuwa kilichofanyika Dodoma kilikuwa ‘kubaka’ demokrasia na kwamba CCM anayoifahamu na iliyomlea sio ile aliyoikuta Dodoma.

CCM wameandika tangazo la mkutano wake na waandishi wa habari kupitia akaunti yao ya Twitter yenye followers zaidi ya 45,000.

 

Diaby Aikacha West Bromwich Albion
Mwinyi Kazimito Ahofia Kucheza Soka Misri