Chama cha Mapinduzi CCM kimejipanga kuyarudisha majimbo yake yaliyochukuliwa na vyama vya upinzani mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuanzisha kampeni ya kuwaondoa wasaliti ndani ya chama hicho.

Hayo yamesemwa na kada wa chama hicho, Anthony Swai alpokuwa akizungumzia mikakati ya chama inayofanywa kwaajili ya kuwaondoa wasaliti.

Amesema kuwa CCM ilishindwa kwa baadhi ya maeneo kutokana na usaliti wa baadhi ya wanachama ambao wamekuwa sio waaminifu.

“Mimi sikubaliani kabisa na hoja ya kuwa katika mkoa wa Kilimanjaro ni ngome ya Chadema, hapana inatokana na wanachama wenzetu kutuzunguka,” Amesema Swai.

Hata hivyo, akizungumzia wasaliti waliokiri makosa yao, Swai amesema kuwa chama kinatakiwa kiwachunguz kiundani zaidi ili kuweza kujilizisha.

 

Ushindi wa Horn kwa Pacquiao wapingwa vikali, Takwimu zaonesha tofauti
JPM anena mazito,asema Serikali itajenga bwawa la umeme