Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapiduzi ya Zanzibar kwa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Christina Mndeme wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za CCM kwa kipindi cha miaka mitano katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa 10 wa CCM jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Christina Mndeme.

Amesema, CCM imeridhika na utekelezaji wa ilani yake baada viongozi mbalimbali kupita katika maeneo yote nchini kukagua utekelezaji wa ilani unaofanywa na serikali zote mbili.

Aidha, Mndeme ameongeza kuwa, malengo ya CCM na Jumuiya zake kwa mwaka 2022 – 2027 ni kusimamia utendaji kazi wa viongozi, maadili ya wanachama, pamoja na kuzisimamia serikali zote kutekeleza sera za na Ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mawakili kukata rufaa hukumu ya maandamano
Makamba, Bi. Koch wajadili ujenzi mradi wa gesi asilia