Ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Mtaa kwa Mtaa ya Mhe . Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana akiwa ameambatana na Mjumbe Kamati ya siasa CCM Nyamagana Comrade Sanyenge pamoja na Katibu wa UVCCM wilaya ya Nyamagana Comrade Malanyingi Matukuta pamoja na Mwenyeji wake Mhe. Haluma Musa Maziko diwani Kata ya Kishiri, amepongezwa na halmashauri Kuu maalum ya Kata ya Kishiri kuwa na ziara zenye tija kwa mustakabali wa maendeleo ya Wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata Kishiri chini ya Mwenyekiti wake Comrade Juvenary Bosco Manji pamoja na mtendaji wa Kata na kikosi Cha Wataalam Ndg. Gerigory Hunja.

Katika kikao hicho kilichodumu kwa saa Moja viongozi hao wamepongeza mfumo wa ziara ya Mtaa kwa Mtaa ambayo inayomfanya Mbunge kukutana na wananchi ana kwa ana kusikiliza na kutatua kero zao ambao ni mfano wa kuigwa na haujawahi kutokea toka Jimbo Hilo liwepo.

Kadharika vioñgozi hao wamepongeza Ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambao unaleta Uwajibikaji kwa serikali za Mitaa na serikali Kuu.

Mhe. Mabula akiwa Kata hiyo anatembelea miradi ya maendeleo 12 ikiwemo Ujenzi wa kituo Cha Afya Fumagira, Shule ya Sekondari Fumagira na Igoma pamoja na Shule nne za Msingi Kanindo, Bukaga, Kishiri pamoja na Bujingwa na kuhitimisha ziara hiyo kwa mikutano mitatu ya hadhara.

Mhe. Mabula katika kikao hicho amepokea kero 36 kwenye sekta ya elimu, Miundombinu ya Barabara, Nishati ya Umeme, Afya, huduma za kijamii kutoka kwa Viongozi waandamizi wa Matawi 7 ya Chama Cha Mapinduzi ya Kata hiyo ikiwa tawi la Ndofe, Kishiri A na B, Bukaga, Kanindo, Kanenwa pamoja na Fumagila pamoja na Wenyeviti wa Mitaa 10 wa Kata hiyo.

Coastal Union bado inaitaka Ligi Kuu
Aragija kupuliza kipyenga Fainali ASFC