Kufuatia kikao kilichofanyika leo na kamati kuu ya CCM, kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, wamemteua Christopher Kajoro Chiza kuwa mgombea wa Ubunge katika jimbo la Buyungu kwa tiketi ya CCM.

Uchaguzi huo ni kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia tiketi ya Chadema, Kasuku Samson Bilago kufariki dunia mnamo Mei 26, 2018.

 

Aidha kwa upande wa vyama vya upinzani, ACT Wazalendo pamoja na Chadema wamekubaliana kuungana kwa heshima ya marehemu Bilago ili kugombea na kulichukua jimbo hilo.

Zitto Kabwe ambaye ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo alisema.

“Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi”.

 

Real Madrid yathibitisha kumuuza Cristiano Ronaldo
Video: Waziri Jafo atangaza ajira 6,180 watumishi afya

Comments

comments