Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kitaibuka na ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo matatu ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu CCM, Humphrey Polepole ambapo amesema kuwa Chama hicho hakina hofu ya ushindi.

Amesema kuwa Chama hicho kimefanya maandalizi makubwa hivyo kwao ushindi ni lazima katika majimbo yote yanayorudiwa uchaguzi.

“Tumekuwa tukifanya tafiti nyingi kuhusu shida za wananchi, na endapo tukifanikiwa kuchaguliwa katika majimbo hayo, kazi kubwa itakuwa ni kwenda kutatua changamoto za wananchi ambazo tayari tumeshazijua,”amesema Polepole

Hata hivyo, amewataka wapiga kura kufuata taratibu zote zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Serikali yaziweka mtegoni shule binafsi
Magazeti ya Tanzania leo Januari 13, 2018

Comments

comments