Katibu wa itikadi na uenezi, CCM, Humphrey Polepole ametangaza ratiba ya kuwapata wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na zanzibar kwa tiketi ya chama hicho.

Amebainisha hayo leo Juni 12, alipokuwa anatoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Bara, amesema tukio la kwanza litakaloanza ni uchukuaji fomu ambalo litaanza tarehe 15 hadi 30 juni maka huu huku tukio la pili, mgombea atakuwa na kazi ya kutafuta wadhamini mikoani ndani ya siku hizohizo 15.

Vikao vya uchujaji vitaanza tarehe 6 hadi 7 julai mwaka huu, ambapo kitaketi kikao cha sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa CCM, kisha julai 8 kitaketi kikao cha maadili na usalama.

Amesema Julai 9 na 10 kamati kuu ya halmashauri na Halmashauri kuu watakuwa na kazi ya kuchuja majina hadi matano na baadae matatu ambayo yatachujwa na mkutano mkuu na kutangaza jina moja.

” Tarehe 11 na 12 julai 2020, utaketi mkutano mkuu wa CCM Taifa ambao wenyewe utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la mwanachama atakaye simama katika uchaguzi wa urais Tanzania kwa tiketi cha chama chetu cha CCM” Amesema Polepole.

Kwa upande wa Zanzibar vikao vya mchujo vitafanyika tarehe 4, na 9 julai, kisha tarehe 10 kikao cha halmashauri kuu ya taifa kitachagua jina moja na mkutano mkuu utaketi kuchuja tarehe 11 hadi 12 julai.

Barakoa si lazima EPL
Mtendaji wa kijiji afutwa kazi na Baraza la Madiwani