Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa tamko rasmi kuhusu adhabu iliyotolewa na Rais John Magufuli kumuondoa aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga katika nafasi hiyo baada ya kuingia bungeni na kujibu maswali akiwa amelewa.

Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka, jana alisema kuwa chama hicho kinampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliouchukua lakini hakitamuadhibu tena Kitwanga kwakuwa adhabu haitolewi mara mbili.

Ole Sendeka alibainisha kuwa uamuzi huo ni fundisho kwa wanachama wengine ambao ni watumishi wa umma kutokiuka miiko ya uongozi.

“Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna kada anayekiuka maadili ya viongozi wa umma,” alisema Ole Sendeka.

Kitwanga aliondolewa katika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ambapo bado alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuhusishwa na sakata la mkataba tata kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Euro 2016: Roman Neustadter Atajwa Kikosini
Makonda azilima Benki zilizopokea mishahara ya watumishi hewa