Chama cha Mapinduzi CCM kimewafungulia baadhi ya makada wake waliokuwa ni wenyeviti wa mikoa wa chama hicho ambao walifungiwa kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt, Bashiru Ally ambapo amesema kuwa chama hicho kimepokea maombi ya kufutiwa adhabu ya kufutiwa uanachama, kwa waliokuwa wenyeviti wa mikoa ambao ni Ramadhani Madabida wa Dar es salaam, Mizengo Kwilasa wa Shinyanga, Christopher Sanya wa Mara na Salum Kondo.

Amesema kuwa Halmashauri Kuu imeazimia kumuweka kwenye uangalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu baada ya kuomba kurudishiwa uanachama baada ya kufuatiwa kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho.

Aidha, katika hatua nyingine, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kimepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, pia kimepokea na kuridhia kanuni mpya za usimamizi wa fedha wa chama hicho pamoja na kumteua, Abdallah Mtolea kuwa mgombea Ubunge kwenye uchaguzi wa marudio, jimbo la Temeke.

Hata hivyo, Mtolea alijiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Temeke na ndani ya Chama cha Wananchi CUF, Novemba 15 katika vikao vya Bunge Jijini Dodoma kwa kile alichokidai kuchoshwa na migogoro ndani ya chama hicho

Live: Rais Magufuli akiweka jiwe la Msingi UPANUZI wa barabara ya Kimara hadi Kibaha
Offset aomba msamaha hadharani