Hatimaye Kamati Kuu ya CCM, imetengua kitendawili cha wagombea ubunge katika majimbo kumi na moja yaliyokuwa yamewekwa kipolo huku ikiwatupa nje mawaziri watatu waliokuwa wakisubiri neema ya Kamati hiyo.

Mawaziri hao ambao majimbo yao yalitajwa kuwa kati ya yale yaliogubikwa na hujuma za rushwa na udanganyifu, ni Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Dr. Tatius Kamani wa jimbo la Busega, waziri wa afya na maendeleo ya jamii, Dk. Seif Rashid wa jimbo la Rufiji na waziri wa Mazingira, Binilith  Mahenge wa jimbo la Makete.

Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye alitaja majimbo tisa kati ya kumi na moja ambayo Kamati Kuu ilikamilisha uamuzi wake na kuwateua wagombea watakaokiwakilisha chama hicho.

CCM

Nape alieleza kuwa majimbo mengine mawili ya mkoani Singida na Manyara bado yanafanyiwa kazi na Kamati Kuu.

Aliwataka wanachama wa chama hicho kuelewa kuwa kushinda kura za maoni pekee sio kigezo cha kupata ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia nafasi hiyo. Hivyo, wawapokee na kuwaunga mkono wanachama walioteuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kugombea ubunge.

“Na ukiangalia kweli wanaotishia kuhamia upande wa pili … kwa sababu kama mnafanya uchaguzi mnamchagua mtu ambaye mnaamini atakwenda kutatua matatizo yenu. Kama wao kupigia upande wa pili kutatua matatizo yao, tunawatakia kila la kheri,” Nape ananukuliwa.

Lowassa: Nitakomesha Wizi Wa Kura, Nchi Itaenda Spidi
Tetesi Za Usajili Wa Wachezaji Barani Ulaya