Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Ethiopia, Tanzania na Rwanda katika michuano ya ubingwa wa wanawake kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amewaambia Waandishi wa Habari katika mkutano wa utambulisho wa Challenge hiyo ya wanawake mjini kampala, kwamba Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Katika sherehe za utambulisho wa michuano hiyo iliyofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Musonye alisema nchi saba zimethibitisha kushiriki Challenge hiyo ya kwanza ya wanawake, itakayofanyika Jinja.

Mbali za Tanzania, Ethiopia na Rwanda Kundi A linaundwa na timu za Uganda, Kenya, Burundi, na Zanzibar na michuano itaanza Septemba 11 hadi 20, 2016.

Middlesbrough Kumsajili Calum Chambers Wa Arsenal
Maafisa wauawa kwa silaha ya kutungua ndege Korea Kaskazini kwa amri ya Rais