Mshambuliaji Cesar Lobi Manzoki amethibitisha atajiunga na klabu inayovaa jezi zenye rangi Nyekundu na Nyeupe, baada ya kumaliza mkataba wake na Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC.

Manzoki anatajwa kuwa kwenye mkakati wa kujiunga na Simba SC ya Tanzania ambayo msimu ujao imedhamiria kurejea heshima ya taji la Ligi Kuu walioipoteza kwa watani zao Young Africans, huku wakitolewa hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Mshambuliaji huyo mwenye uraia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwa kutaja rangi.

Manzoki ameandika: “Red and White (Nyekundu na Nyeupe)”

Inadaiwa kuwa Manzoki ambaye ni mzaliwa na DR Congo ameshawasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu wa kujiunga na Simba SC, huku akitajwa kuwa mrithi wa nafasi ya Mshambuliaji kutoka Rwanda Meddie Kagere.

Jana Jumatatu (Juni 27) Manzoki aliwaaga rasmi Viongozi, Wachezaji na Mashabiki wa klabu ya Vipers SC ya Uganda.

Wakimbizi 46 wafariki ndani ya lori
Hassan Bumbuli: Dar24 Media mmetupa mafanikio haya