Kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas amepuuza taarifa za kutaka kuondoka Stamford Bridge baada ya kutemwa kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea ambacho kilipambana na West Ham Utd usiku wa kuamkia jana jijini London.

Fabregas aliripotiwa kukasirishwa na mpango wa meneja wa Chelsea Antonio Conte kumuweka benchi na kufikia hatua ya kutaka auzwe, huku klabu za Real Madrid na Juventus zikitajwa kuwa tayari kumsajili katika kipindi hiki.

Kwa nyakati tofauti mashabiki wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 walikua wakimuuliza maswali kupitia mitandao ya kijamii kuhusu fununu za kuwa tayari kuihama Chelsea, lakini hakujibu chochote.

Hata hito meneja wa Chelsea Antonio Conte alisisitiza kuwa, Fabregas bado ni mchezaji wa The Blues na itaendelea kuwa hivyo.

Alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo dhidi ya West Ham Utd, meneja huyo kutoka nchini Italia alisema haoni sababu ya suala la kiungo huyo kuwekwa benchi kuwa gumzo hadi kufikia hatua ya kuhusishwa na mipango ya kutaka kuuzwa.

Fabregas, aliwasjiliwa na Chelsea akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona kwa ada ya uhamisho ya Pauni milion 30 mwaka 2014, na katika msimu wake wa kwanza klabuni hapo alikuwa sehemu ya waliosaidia kutwaa ubingwa wa England pamoja na Capital One Cup.

Chelsea Yajaribu Tena Kwa Kalidou Koulibaly
Hali Yaendelea Kuwa Tete Kwa Joe Hart, Guardiola Atoa Baraka