Shujaa wa mchezo wa kombe la ligi kati ya Chelsea dhidi ya Leicester City Cesc Fabregas ametoa maneno ya kejeli kwa waandishi wa habari baada ya kusakamwa kwa kipindi cha majuma kadhaa tangu kuanza kwa msimu wa 2016/17.
Fabregas alifunga mabao mawili ya ushindi katika mchezo wa kombe la ligi uliomalizika kwa wenyeji Leicester City kukubali kisago cha mabao manne kwa mawili, amesema hatua hiyo itawaziba midomo waandishi waliokua wanamsakama kwa kipindi kirefu.
Kiungo huyo kutoka nchini Hispania, alifunga mabao hayo katika muda wa nyongeza baada ya kushuhudia dakika 90 zikimalizika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu ya kufungana mabao mawili kwa mawili.
Fabregas amesema hatua hiyo inadhihirisha bado ana uwezo mkubwa wa kuitumikia Chelsea ambayo kwa sasa ipo mikononi mwa meneja Antonio Conte, ambaye hajaonyesha kuwa tayari kumtumia kwenye kikosi cha kwanza katika michezo ya ligi ya nchini England.
“Nimefarijia kuwa sehemu ya kikosi tangu mwanzo wa mchezo hadi mwisho, na nimeonyesha nina uwezo wa kuisaidia timu,” Alisema Fabregas alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports.
“Natumai jambo hili litawaziba midomo waandishi wa habari waliokua wanaandika na kusema maneno mabaya dhidi yangu…
“Nafahamu nini nitakachokifanya katika timu hii pindi nitakapopewa nafasi ya kucheza.”
Mabao mengine ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na Gary Cahill na Cesar Azpilicueta huku Shinji Okazaki akipachika mabao mawili yaliyowafuta machozi Leicester City.
Matokeo ya michezo mingine ya kombe la ligi iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko England.
Bournemouth 2 – 3 Preston
Brighton 1 – 2 Reading
Derby 0 – 3 Liverpool
Everton 0 – 2 Norwich
Leeds 1 – 0 Blackburn
Newcastle 2 – 0 Wolves
Nottm Forest 0 – 4 Arsenal
Michezo ya michuano hiyo itakayochezwa hii leo.
Fulham v Bristol City (Craven Cottage)
Northampton v Man Utd (Sixfields Stadium)
QPR v Sunderland (Loftus Road Stadium)
Southampton v Crystal Palace (St. Mary’s Stadium)
Swansea v Man City (Liberty Stadium)
West Ham v Accrington (London Stadium)
Stoke v Hull (bet365 Stadium)
Tottenham v Gillingham (White Hart Lane)