Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Rungwe, Mbeya kimemfukuza uanachama na kumvua udiwani, Diwani wake wa Kata ya Kambasegela, Kiswigo Mwakalebela kwa madai ya kukiuka taratibu na kanuni za chama hicho.

Hata hivyo, Mwakalebela mwenyewe amesema amejivua uanachama na kuhamia CCM kwa madai kuwa anashindwa kufanya kazi kwa kuwa amezungukwa na viongozi wengi wa CCM.

Naye wenyekiti wa Chadema halmashauri ya Busokelo, Furaha Mwakalundwa amesema kuwa baada ya kujiridhisha kupitia intelijensia ya chama hicho kuhusiana na mwenendo wa Mwakalebela walibaini amekuwa akiivunja katiba ya Chadema hivyo hawawezi kumvumilia.

“Chama kina taratibu na falsafa zake na chama hiki ni kikubwa kuliko mtu na diwani anapatikana kwa misingi ya Chadema hivyo inapotokea mtu unavunja na kukiuka katiba ya chama, basi hatuna budi kumchukulia hatua na ndicho kilichotumika kwa huyu mwenzetu Mwakalebela,” amesema Mwakalundwa.

 

Hata hivyo, kwa upande wake Mwakalebela amesema hana taarifa za kufukuzwa na chama chake bali ameamua kujivua uanachama na udiwani kwa hiyari yake baada ya kuona anashindwa kumudu kuwatumikia wananchi kutokana na kukosa ushirikiano na viongozi ngazi za vijiji na vitongoji.

Kalanga aivuruga CCM Monduli, wengine wakimbilia Chadema
Danny Ings aikacha Liverpool dakika za lala salama