Vijana wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro wametamba kushiriki maandamano na mikutano kama sehemu ya operesheni UKUTA iliyotangazwa na chama hicho, Septemba 1 mwaka huu.

Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Kilimanjaro, Kibona Dickson amesema kuwa vijana wa mkoa huo wamejipanga kushiriki maandamano hayo ambayo amedai yatamalizikia mjini Moshi, licha ya kuwepo kwa katazo la Jeshi la Polisi.

Dickson amesema kuwa hawaogopi katazo la Polisi na Serikali akidai kuwa kushiriki oparesheni hiyo ni sehemu ya majukumu yao na wanalindwa na katiba na sheria za nchi.

“Tulifurahi sana kupokea tamko la kushiriki maandamano kwa sababu ni wajibu wetu na haki yetu ya msingi kuilinda demokrasia,” Dickson anakaririwa.

Alisema kuwa wanasikitishwa na ukimya wa msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi kuhusu makatazo ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa ambayo amedai ni kinyume cha sheria ya vyama vya siasa yam waka 1992, kifungu cha 5.

Jeshi la Polisi limetahadharisha mtu yeyote atakayeshiriki oparesheni hiyo na tayari viongozi wa ngazi za juu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho wameshahojiwa na jeshi hilo.

TRA Yazindua Zoezi La Uhakiki,Uboreshaji Taarifa Za Mlipa Kodi
Wimbo Mpya: Nay wa Mitego feat Tiki - Good Time